Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar ndugu Amour Hamil Bakari akifanya ziara katika maeneo mbali mbali ya biashara katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, lengo likiwa ni kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo walipakodi katika Mkoa huo.

Katika ziara hiyo Kamishna alitembelea Bandari ya Wete pamoja na baadhi ya Walipakodi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.