BODI YA MAPATO ZANZIBAR (ZRB), INAWATANGAZIA WALIPAKODI NA WANANCHI KWA UJUMLA KWAMBA, KUFUATIA KUTIWA SAINI KWA SHERIA YA FEDHA NAMBARI 9 YA MWAKA 2018 YA “SHERIA ZA KUTOZA KODI NA KUBADILISHA BAADHI YA SHERIA ZA FEDHA NA KODI KUHUSIANA NA UKUSANYAJI NA UTHIBITI WA MAPATO YA SERIKALI NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO”, TAREHE ZA KUWASILISHA RITANI NA MALIPO YA KODI ZIMEBADILIKA:

KWA MABADILIKO HAYO, ZRB INATANGAZA RASMI KWAMBA KUANZIA JULAI 2018, TAREHE YA MWISHO YA KUWASILISHA RITANI NA MALIPO YA KODI ITAKUWA NI KABLA AU NDANI YA TAREHE ISHIRINI (20) YA KILA MWEZI BAADA YA KIPINDI CHA KUFUNGA HESABU (YAANI BAADA YA MWEZI WA BIASHARA).

MABADILIKO HAYA YAMEFANYIKA CHINI YA VIFUNGU VYA 18 NA 31 VYA SHERIA YA USIMAMIZI WA KODI NAMBARI 7 YA MWAKA 2009.

TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR.

LIMETOLEWA NA KITENGO CHA MAHUSIANO KWA UMMA

BODI YA MAPATO ZANZIBAR.