The Fourth Corporate Plan (CP4) focuses on ā€œStrengthening Tax Administration Through Modernizationā€. Modernization of systems and processes through innovation in Information and Communication Technology (ICT) that transforms organizational processes, promote operational efficiency and improve service delivery.

This Corporate Plan lays a foundation on how the Zanzibar Revenue Board (ZRB) intends to achieve its objectives and aspirations during the period. The Plan has outlined vision and mission that will provide impetus for achieving tangible results. Critical and valuable lessons were observed from the Third Corporate Plan (CP3) and have been incorporated in this Plan.  

The ZRB enters its Fourth Corporate Plan to optimize collection of Government revenues and meet the ZRB vision and mission. The implementation of the Plan will involve carefully translating the corporate objectives into actions with very specific strategic initiatives. Other actions will involve creating awareness among staff, key stakeholders and development partners. 

The Corporate Plan focuses on key strategic areas which include: optimization of revenue collection; improvement of quality of services and compliance; innovation in digitization and technology harness; and improvement of staff performance. 

 

Mpango Mkakati wa Nne wa ZRB (2020/2021 - 2024/2025)

Mpango wa Mkakati wa Nne (CP4) unazingatia "Kuimarisha Usimamizi wa Kodi Kupitia Mageuzi". Uboreshaji wa mifumo na taratibu za kazi kwa kutumia uvumbuzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayobadilisha taratibu za kazi za Taasisi, kukuza ufanisi wa utendaji na kuboresha utoaji wa huduma.

Mpango Mkakati huu unaweka msingi juu ya jinsi Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) inavyokusudia kufikia malengo na matarajio yake katika kipindi hicho. Aidha, Mpango umeelezea DIRA (maono) na DHAMIRA ambayo itatoa msukumo wa kufikia matokeo yanayoonekana. Mafunzo muhimu kutokana na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu wa ZRB (CP3) yamezingatiwa na yameingizwa katika Mpango huu.

ZRB inaingia katika utekeelezaji wa Mpango Mkakati wake wa Nne kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kufikia Dira (maono) na dhamira ya ZRB. Utekelezaji wa Mpango utahusisha kutafsiri kwa uangalifu malengo ya Taasisi kwa vitendo na mipango maalum ya kimkakati. Vitendo vingine vitajumuisha kukuza uelewa kati ya Wafanyikazi, Wadau muhimu na Washirika wa Maendeleo.

Mpango Mkakati unazingatia maeneo muhimu ya kimkakati ambayo ni pamoja na: ongezeko la ukusanyaji wa mapato; uboreshaji wa huduma na uwajibikaji; uvumbuzi katika matumizi ya dijitali na teknolojia; na uboreshaji wa utendaji wa wafanyikazi.