Kufuatia tangazo la ajira lililotolewa na ZRB hivi karibuni ambalo lilihusu kuitwa kwa waombaji wa ajira ya kufanya usaili wa kujaza nafasi mbali mbali za kazi katika ofisi za ZRB, kumejitokeza watu wasiokuwa waaminifu na wenye nia ya kufanya vitendo vya ulaghai kwa walioomba ajira hizo.

ZRB imekuwa ikipokea malalamiko ya kuwepo watu wanaojifanya aidha ni wafanyakazi wa ZRB au wana ushawishi wa karibu na Uongozi. Watu hao wamekuwa wakiwatoza watu pesa kwa viwango tofauti wakidai kuwa watawapatia ajira.

ZRB inawatabainisha wananchi wote kuwa watu hao ni matapeli na wananchi wanapaswa kuwaepuka. Na kwamba hakuna mtu yoyote awe ni mfanyakazi wa ZRB au mwengine yeyote ambaye anaweza kutoa ajira kwa waombaji kinyume na utaratibu uliopangwa.

ZRB inaijuilisha jamii kuwa inatumia njia rasmi za uajiri na za mawasiliano katika mchakato mzima wa ajira. Hivyo, wananchi wanapaswa kuwapuuza wale wote ambao wanafanya vitendo hivyo ambavyo si  tu kuwa si vya kizalendo, bali pia vyenye nia yakuchafua jina na haiba ya ZRB.

Aidha, ZRB inatoa onyo kali kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo, na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR.