Taarifa ya Kuongeza Muda wa Kulipa Kodi ya Mwezi September 2025
Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) inawajuilisha Walipakodi wote kuwa, tarehe ya mwisho ya kufanya Malipo yα Kodi ya Mwezi wa Septemba 2025 imeongezwa muda kutoka tarehe 20 Oktoba hadi tarehe 22 Oktoba 2025.
Walipakodi wote ambao hawajafanya malipo wanahimizwa kutumia muda wa ziada kukamilisha malipo ya Kodi kwa wakati ili kuepuka usumbufu.


