Hongera ZRA kwa Kuvuka Malengo

Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) imesema imevuka malengo ya makusanyo ya kodi kwa asilimia 103.31 ambapo kwa kipindi cha mwezi Septemba ilikadiriwa kukusanya shilingi bilioni 74.049 na imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 76.467.