Matunda ya Kodi - Soko la Jumbi

Soko la Jumbi lilifunguliwa rasmi tarehe 27/10/2024 na kwa sasa tayari wafanyabiashara wameanza kufanya biashara zao katika soko hilo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi  wakati wa kampeni zake alitoa ahadi ya kuwaimarisha wajasiriamali kwa kuwajengea masoko makubwa ya kisasa.

Soko la Jumbi linauwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 500 kwa wakati mmoja .