TAARIFA YA MAKUSANYO 2023/2024
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya Sh. Trilioni 7.53 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25, sawa na ufanisi wa asilimia 101.32 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 7.43.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda imeeleza kuwa ufanisi wa makusanyo ya Robo ya Tatu ya mwaka 2024/2025 ni sawa na ukuaji wa asilimia 13.47 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 6.63 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2023/24.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa makusanyo yaliyokusanywa katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25 yanapelekea TRA kuweza kuweka rekodi ya kipekee katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kufikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa miezi 9 mfululizo katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Taarifa ya Bw. Mwenda inafafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Julai – Machi, mwaka wa fedha 2024/25, TRA imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 24.05 sawa na ufanisi wa asilimia 103.62% ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni



